Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Tajamu Ulama Jabal Amil katika taarifa yake ilitoa shukrani na pongezi zake kwa nchi ya Iran, uongozi wake na wananchi wake kwa sababu ya misimamo yake thabiti katika kuunga mkono masuala ya haki, na ikatuma salamu za heshima kwa uongozi wa muqawama ambao kwa mara nyingine umethibitisha kuwa uthabiti wake si jambo la mpito, bali ni mtazamo uliokita mizizi katika kukabiliana na uchokozi.
Mkusanyiko huo unaamini kuwa usitishaji wa mapigano ulipatikana kutokana na ustahimilivu wa wapiganaji, mapambano yao ya kishujaa na ya kipekee, pamoja na msaada wa uongozi wa Wilayat al-Faqih na maafisa wa Iran kwa njia hii, na kwa baraka za damu ya mashahidi na subira ya Walebanon waadilifu ambao, licha ya ugumu wa changamoto, hawakuacha chaguo la heshima na hadhi.
Taarifa hii pia iliisifu sana nafasi ya uongozi wa muqawama na makundi mengine ya kitaifa ya Lebanon, na ikatuma salamu zake kwa Walebanon wote walio huru waliodumu imara, wakaunga mkono na kutoa msaada, pamoja na mataifa yote hai duniani ambayo kwa dua na msaada wao yalikuwa pamoja nasi na kila mmoja kwa nafasi yake akashiriki katika mafanikio haya.
Katika suala la ndani, Tajammu Ulama Jabal Amil ilimtaka rais, waziri mkuu na serikali kurekebisha misimamo yao, kurejea kutoka njia ya kumridhisha adui na kutafuta ridhaa yake, na kurekebisha kosa walilofanya kwa kuuhalalisha uhalifu dhidi ya muqawama na kuulaumu, kwa kupitia upya maamuzi yaliyotolewa, kwa roho ya uwajibikaji na uwazi, kwa namna itakayolinda maslahi ya juu ya taifa.
Taarifa hii ilisisitiza kuwa, ni muhimu kutumia uwezo wa muqawama na utayari wake, pamoja na nafasi ya jeshi la Lebanon, ili jeshi liweze kutekeleza jukumu lake la asili la kulinda nchi na kukabiliana na uvamizi.
Pia Tajammu Ulama Jabal Amil iliwataka wananchi wapendwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na taasisi husika, hasa yale yanayohusiana na kutotoa huduma yoyote ya bure kwa adui, iwe kupitia upigaji picha au uzembe kuhusu mabaki ya uchokozi; kwani mambo haya yana hatari kubwa kwa umma.
Taarifa hii ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha mshikamano wa kijamii miongoni mwa watu, kwa sababu msaada wa kimaadili, roho ya ushirikiano na kusaidiana kati ya wanajamii, vyote ni nguzo muhimu za kuvuka athari za hatua hii nyeti.
Maoni yako